Multilingual Scriptures Home » Swahili New Testament » Philemon
Swahili New Testament | ||
Chapter # | Verse # | Verse Detail |
1 | 1 | Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu |
1 | 2 | na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkupo. |
1 | 3 | Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana yesu Kristo. |
1 | 4 | Kila wakati ninaposali nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru Mungu |
1 | 5 | maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana wetu Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu. |
1 | 6 | Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo. |
1 | 7 | Ndugu, upendo wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu. |
1 | 8 | Kwa sababu hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako katika Kristo, kukuamuru ufanye unachopaswa kufanya. |
1 | 9 | Lakini kwa sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya hivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake. |
1 | 10 | Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni. |
1 | 11 | Ni Onesimo yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu, lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia. |
1 | 12 | Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe. |
1 | 13 | Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Habari Njema. |
1 | 14 | Lakini sitafanya chochote bila kibali chako. Sipendi kukulazimisha unisaidie, kwani wema wako unapaswa kutokana na hiari yako wewe mwenyewe na si kwa kulazimika. |
1 | 15 | Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi uweze tena kuwa naye daima. |
1 | 16 | Na sasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi ya mtumwa: yeye ni ndugu yetu mpenzi. Na wa maana sana kwangu mimi, na kwako atakuwa wa maana zaidi kama mtumwa na kama ndugu katika Bwana. |
1 | 17 | Basi, ikiwa wanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokee tena kama vile ungenipokea mimi mwenyewe. |
1 | 18 | Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwa na deni lako, basi, unidai mimi. |
1 | 19 | Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: yako.) |
1 | 20 | Haya, basi, ndugu yangu, nifanyie jambo hilo kwa ajili ya jina la Bwana; burudisha moyo wangu kama ndugu katika Kristo. |
1 | 21 | Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba. |
1 | 22 | Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini kwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni. |
1 | 23 | Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu, anakusalimu. |
1 | 24 | Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu, wanakusalimu. |
1 | 25 | Nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. |